USIKUBALI HOFU IKUIBE AMANI YAKO USIKUBALI HOFU IKUIBE AMANI YAKO USIKUBALI HOFU IKUIBE AMANI YAKO

Published by: DivinityTV
10/11/2026 10:41 AM
Views: 2

 

HELLO RAFIKI! JE WAJUA?

USIKUBALI HOFU IKUIBE AMANI YAKO

 Wafilipi 4:6–7 "Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu."

Najua kuna nyakati moyo unachoka, mawazo yanakuwa mengi, na kesho inaonekana kutisha. Huenda unapitia changamoto ambayo hujui itakuwaje, au unaomba jambo ambalo bado hujaona majibu yake.

Lakini  usisahau kwamba hata unapokosa majibu, bado Neema ipo. Usiruhusu hofu itawale moyo wako. Mkabidhi Mungu mizigo yako, endelea kuomba na usisahau kumshukuru kwa wema wake.

Mungu hakutuahidi kwamba hatutapitia changamoto, lakini Neno lake linatukumbusha kwamba tunaweza kupata amani yake katikati ya changamoto hizo.

Leo natamani niombe nawe sala hii !! Rudia nyuma yangu:---

Baba yangu wa mbinguni, nimechoka kubeba mizigo hii moyoni mwangu. Leo naiweka mikononi mwako. Ninakushukuru kwa upendo na rehema zako. Nipe nguvu ninapodhoofika, tumaini ninapokata tamaa, na amani pale hofu inapojaribu kunitawala. Nisaidie kukuamini hata kabla sijaona majibu. Katika jina la Yesu Kristo, Amina!_

.....Ikiwa ujumbe huu umegusa moyo wako, usiishie kuusoma peke yako. *Mtumie mtu mmoja unayempenda, rafiki anayepitia magumu, au mtu ambaye huenda anatabasamu mbele za watu huku akilia moyoni.* Huenda maneno haya yakamkumbusha kwamba bado kuna tumaini na kwamba hajakatazwa kumwendea Mungu kwa mahitaji yake.

 

*Sambaza ujumbe huu. Kuwa sababu ya mtu mwingine kupata faraja leo!

 

Rev Christian

SHALOM!  Yesu Yupo

News videos

News images